Matthew 6:22-23

Jicho Ni Taa Ya Mwili

(Luka 11:34-36)

22 a “Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni nyofu, mwili wako wote utajaa nuru. 23 bLakini kama jicho lako ni ovu, mwili wako wote utajawa na giza. Kwa hiyo basi, kama nuru iliyomo ndani yako ni giza, hilo ni giza kuu namna gani!

Copyright information for SwhNEN